Connect with us

Makala

Tupo Tayari-Gamondi

kocha wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema wamejipanga vizuri kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Asas Fc  licha ya kutokujua uimara na udhaifu wa wapinzani wao.

Kesho Agosti 20 katika Uwanja wa Azam Complex klabu hiyo itacheza mchezo wa wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika mchezo utakaowakutanisha na mabingwa wa Ligi ya Djibouti Asas Fc.
Gamondi raia wa Argentina amesema yeye ni kocha mpya na anatamani kuweka historia yake mpya ikiwa Yanga haijaingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa inahistoria ya kutoingia makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka ya hivi karibuni.

“Tumejipanga vizuri, hatumfahamu mpinzani kiundani lakini tumejipanga kufanya vizuri na kuandika historia mpya”.

“Tunakwenda kuiwakilisha Yanga na Tanzania kwa ujumla, naamini kesho tutakuwa na mchezo mzuri na kuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi ya Mabingwa” Miguel Gamondi.

Pia sambamba na kocha huyo beki wa klabu hiyo Nickson Kibabage amesema kuwa klabu hiyo imejipanga vilivyo kwa ajili ya mchezo huo na hawatawadharau wapinzani wao hata kidogo.

“Hatudharau mpinzani. Unapokutana na mpinzani kwenye Ligi ya Mabingwa bila shaka anakuwa amefanya vizuri alipotoka, tutakwenda kwa umakini mkubwa na kufanyia kazi yale ambayo kocha ametuelekeza” Nickson Kibabage

Yanga sc itacheza na Asas Fc jijini Dar es salaam kwa michezo yote miwili ya hatua ya awali ambayo itafanyika katika uwanja wa Chamazi Complex kutokana klabu hiyo kukosa uwanja wenye vigezo vya Caf nchini mwao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala