Connect with us

Makala

Kocha Yanga Queens Atua Biashara United

Aliyekuwa kocha wa muda mrefu wa klabu ya soka ya Wanawake ya Yanga queens Edna Lema amaejiunga na klabu ya Biashara United ya mkoana Mara kama kocha msaidizi wa klabu hiyo ambayo inashiriki ligi kuu daraja la kwanza.

Kocha huyo amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo atakua msaidizi wa kocha mkuu Amani Josiah huku pia akiungana na Ivo Mapunda ambaye ni kocha wa makipa wa klabu hiyo.

Imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu kufundisha soka la wanaume na hatimaye leo inaenda kutimia, Kwangu inaenda kuwa changamoto mpya. Ingawa haitokuwa jambo rahisi lakini nipo tayari”

“Mkataba wangu ni wa mwaka mmoja na jukumu letu kubwa pamoja na hamu ya wana mara ni kuhakikisha klabu ya Biashara inarejea kwenye ligi kuu Tanzania Bara”.Alisema Edna ambaye ni maarufu kwa jina la Edna Lema Mourinho

Edna amekua akizifundisha timu nyingi za wanawake nchini ambapo ikiwa ni takribani miezi tisa bila kuwa na timu ya kufundisha tangu alipoachana na Yanga Princess Desemba 8, 2022 klabu hiyo ilipovunja mkataba wake pamoja na msaidizi, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ na timu kupewa Fredy Mbuna.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala