Connect with us

Makala

Ajibu Atua Coastal Union

Klabu ya Coastal Union imetangaza kukamilisha usajili wa Ibrahim Ajibu ambaye alikua ni mchezaji huru baada ya kutemwa na klabu ya Singida Fountain Gate alipojiunga akitokea katika klabu ya Azam Fc.

Ajibu ambaye anatambulika kwa kipaji chake hasa akiwa katika klabu ya Yanga sc ambayo aliichezea kwa msimu mmoja na kisha kujiunga na Simba sc sehemu ambayo hakufanikiwa kupata namba kikosi cha kwanza.

Mchezaji huyo tayari ameshajiunga na timu hiyo katika kambi ya mazoezi iliyoko eneo la usagara na tayari ameshatambulishwa rasmi na mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Usajili wa kiungo huyo mshambuliaji umekuja kutokana na pendekezo la kocha Mwinyi Zahera ambaye alimfundisha akiwa katika klabu ya Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala