Connect with us

Makala

Kapombe,Tshabalala Wajifunga Simba sc

Wachezaji Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wameongeza mikataba mipya kuendelea kusalia katika klabu ya Simba sc kwa misimu miwili zaidi na kuzima tetesi za kutakiwa na timu za nje ya nchi.

Simba sc imeendelea na maboresho ya kuongeza wachezaji wapya klabuni hapo huku pia ikifanikiwa kuwabakisha mastaa hao ambao wameonyesha viwango vikubwa kwa zaidi ya misimu mitano sasa wakifanikiwa kuwaweka benchi mpaka mastaa wa kigeni wanaokuja klabuni hapo katika nafasi zao.

Simba sc imeendelea kufaidi ubora wa Kapombe tangu imsajili kutokea Azam Fc japo amekua akisumbuliwa na majeraha kadhaa lakini amekua na kiwango kizuri anapokua uwanjani.

Mohamed Hussein tayari alikua na ofa kutoka nchini Afrika ya kusini lakini uimara wa Simba sc kiuchumi msimu huu umekua nguzo kubwa kwa klabu hiyo kumbakisha staa huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala