Connect with us

Makala

Beki Mpya Atua Azam Fc

Haipoi Haiboi ndiyo msemo wanaousema mashabiki wa Azam fc baada ya klabu hiyo kuendelea kushusha vyma vya nguvu ka ajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini ambapo wamefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji  Cheikh Tidiane Sidibe akitokea Teungueth inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Senegal.

Beki huyo wa kushoto amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo akiungana na kocha wake wa zamani wa klabu yake ya Teungueth Yousuph Dabo ambaye ametua Azam Fc tangu msimu uliopita lakini msimu huu ndio wa kwanza kwake kama kocha wa klabu hiyo.

Azam Fc baada ya kumtambulisha staa huyo ndio imemaliza usajili wake kama ilivyotangaza kuwa itasajili mastaa wanne pekee katika dirisha hili ambapo mmoja ni mzawa Feisal Salum huku beki huyo anaungana na Gibril Sillah na Alasane Diao kukamilisha usajili klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala