Connect with us

Makala

Klabu ya Simba sc imeachana na mpango wa kumsajili mlinzi wa katikati wa klabu ya Asec Mimosas Souleymane Coulibaly kutokana na dau kubwa la usajili kutoka kwa klabu hiyo.

Licha ya klabu hiyo kuonyesha ushirikiano wa kiutosha kutokana na hitaji la Simba sc mpaka sasa Simba Sc wapo kimya huku kukiwa na taarifa Kuachana na Mlinzi huyo kwa madai ya ada kubwa ya usajili iliyowekwa na klabu hiyo.

Simba sc pamoja na kukaa huko kimya bado wanaangalia kama wanaweza kupata beki mwingine wa bei nafuu ili kupunguza gharama ikizingatiwa pia bado wanaye Joash Onyango ambaye mpaka sasa bado hatima yake haijafahamika kutokana na kutopatikana kwa bei hitajika ama kutoafikiana kuvunja mkataba wake uliosalia.

Pamoja na hayo endapo Simba sc itapata beki mwingine wa ndani basi moja kwa moja inaweza kuachana na usajili wa beki huyo anayekichafua vizuri katikati kiasi cha kuifanya klabu yake kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala