Connect with us

Makala

Mgunda Anukia Simba Queens

Mabosi wa klabu ya Simba sc wana mpango wa kumhamishia kocha Juma Mgunda kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba queens ili kupisha nafasi ya kocha Roberto Oliveira kuja na kocha msaidizi ambaye anamtaka ili kupata uhakika wa kuleta makombe zaidi klabuni hapo.

Robertinho amewaomba mabosi wa klabu hiyo aje na wasaidizi wake akianza kuja na kocha wa viungo kutoka Rwanda Hategekimana Corneille na sasa analeta msaidizi wake hivyo kuwalazimu mabosi wa klabu hiyo kufanya maamuzi hayo mazito ya kufyeka benchi la ufundi wakianza kuwaondoa Seleman Matola na Patrick Rweyemamu.

Pia kumekua na tetesi za kocha huyo kutaka kurejea Coastal Union ambapo amezakanusha kabisa huku akisema kuwa bado ana mkataba na Simba sc.

“Mmefanya vizuri kuniuliza, kwani majibu yangu yatawapa kujua bado ni mfanyakazi wa Simba. Kuhusu Coastal siwezi kukataa kwamba ni timu yangu ambayo nimetoka nayo mbali, tukirekebisha matatizo yetu tutaendelea salama,” alisema kocha huyo ambaye amejiwekea rekodi nzuri Simba.

“Nipo Tanga kwa mapumziko utakapofika muda wa kurejea kwenye majukumu Simba mashabiki wangu wataniona,”alisema na kuongeza kuwa msimu uliomalizika aliuona ushindani mkubwa ambao unawapa picha ya kufanya maandalizi makubwa zaidi kwa ajili ya ujao.

“Ligi ina ushindani mkali na soka linakuwa, hivyo kila timu itakuwa inajipanga kulingana na mahitaji yake ya msimu mwingine,” alisema Mgunda

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala