Connect with us

Makala

Manula Afanyiwa Upasuaji

Hatimaye golikipa namba moja wa Simba sc na Timu ya Taifa ya Tanzania Aishi Manula amefanyiwa upasuaji goti salama ili kutibu majeraha yake yaliyokua yakimsumbua na kusababisha kukosa michezo kadhaa ya ligi kuu na ile ya kimataifa.

Kipa huyo aliibukia katika klabu ya Azam Fc kisha akijiunga na Simba sc amefanyiwa upasuaji huo nchini Afrika ya kusini ambapo sasa atapewa mapumziko ya siku chache kisha atarejea nchini kuendelea na matibabu akisubiri kupona kabisa.

Manula amekua msaada mkubwa kwa klabu yake ya Simba sc na Taifa kwa ujumla huku akiwa ni moja ya makipa bora wa ligi kuu akichukua tuzo hiyo mara kadhaa.

Simba sc ilitoa taarifa kuwa ina mpango wa kumpeleka katika matibabu kipa huyo ili apone kabisa kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala