Connect with us

Makala

300m Zambakisha Beki Simba sc

Kiasi cha shilingi milioni mia tatu zilizotolewa na mabosi wa Simba sc zimefanikiwa kumbakisha beki Mohamed Hussein aliyekua na mpango wa kutimkia katika klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika ya kusini.

Beki huyo tegemeo wa timu ya Taifa ya Tanzania alikua yupo mwishoni mwa mkataba wake klabuni hapo huku tayari akiwa na ofa nono ya Kaizer Chiefs waliokua wameweka kiasi cha milioni mia nne na mshahara wa milioni thelasini za kitanzania.

Mabosi wa Simba sc wakitumia nguvu kubwa ya ushawishi wamefanikiwa kuzima dili hilo na kumsainisha dili hilo jipya lenye thamani ya shilingi milioni mia kila mwaka kwa miaka mitatu huku wakimpatia mshahara wa shilingi milioni kumi kwa mwezi.

“Haikuwa rahisi kwani, tayari Tshabalala alikuwa na ofa kubwa lakini viongozi wamekaa naye na kufanikiwa kumshawishi ili aweze kuendelea kuitumikia Simba kwa mafanikio kama alivyofanya tangu amejiunga na timu hii akitokea Kagera Sugar,”Alisema mtu wa ndani wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala