Connect with us

Makala

Yanga sc Yagomea Faini Caf

Kufuatia kuamuriwa kulipa faini ya zaidi ya Tsh.80 milioni klabu ya Yanga sc imeamua kukata rufaa uamuzi wa shirikisho hilo barani Afrika kuitoza klabu hiyo faini kufuatia baadhi ya makosa katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria.

Yanga sc iliamriwa kulipa faina ya dola elfu 10 kwa kosa la mashabiki wake kuwasha mafataki na moto wakati wa mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa huku pia ikipigwa faini ya dola elfu 25 kwa kosa la timu ya Rivers kuibiwa kiasi cha dola elfu tano pamoja na basi la timu hiyo kukutwa na harufu inayodhaniwa kuwa ni kemikali hatarishi.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu hiyo ni kwamba klabu hiyo imeamua kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Caf ambao pia kikanuni wanaruhusiwa kukata rufaa ndani ya siku tatu za kazi tangu uamuzi huo utolewe huku kama wanakubaliana na adhabu basi wanapaswa kulipa fedha hiyo ndani ya siku sitini.

Katika moja ya mambo yatakayoainishwa katika utetezi huo ni  kuwa klabu hiyo haiusiki na pesa zilizoibiwa ndani ya basi la wageni wao ambao walikuwa ni Rivers United kama Caf walivyodai kwenye barua.

“Ni kweli tumepokea Barua ya kutozwa faini Dollar 35,000 kwa makosa ya kuwasha fataki, Moshi na Tochi uwanjani pamoja na Basi la Rivers Utd kuvamiwa”

“Baadhi ya Matukio yanafanywa sana na Wenzetu waarabu lakini huoni wakidhibiwa hivyo Wananchi tunawaomba Waache hizi tabia kwasababu tupo hatua nzuri ambayo inawezekana tunajaribiwa kutolewa kwenye ‘focus’ tunaomba Wananchi waache hizi tabia ili tusiwape sababu”Alisema Ally Kamwe

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala