Connect with us

Makala

Wydad Watua Kibabe

Kikosi cha klabu ya Wydad Casablanca kimewasili nchini jioni ya leo kwwa ajili ya mchezo wa siku ya Jumamosi wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Simba sc utakaofanyika saa kumi jioni katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Msafara wa kikosi hicho umewasili na kupokelewa na maafisa wa klabu ya Simba sc sambamba na waandishi wa habari waliokua wakichukua picha na kufanya mahojiano na baadhi ya mastaa wa klabu hiyo hasa wale wanaojua kiingereza na kiswahili.

Wydad AC wametua  leo  wakiwa na msafara wa watu 50 na wamekuja na ndege ya kukodi moja kwa moja kutoka nchini Morroco mpaka hapa nchini huku baadhi ya mabosi wa klabu hiyo wakiwa wameshawasili tangu siku ya Jumamosi kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.

Baada ya mchezo huo Simba sc italazimika kusafiri kwenda nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano ukaofanyika Jumamosi ya April 30 mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala