Connect with us

Makala

Musonda Aomba Radhi

Mhambuliaji wa klabu ya Yanga sc Kennedy Musonda amewaomba radhi mashabiki wa klabu yake ya Yanga sc kufuatia timu hiyo kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba sc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika wikiendi iliyopita katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Staa ambaye ni raia wa Zambia aliyesajili na Yanga sc katika dirisha dogo la mwezi januari amewashukuru pia mashabiki wa klabu hiyo kwa kuendelea kuwasapoti huku akiahidi kuwa watarejea kwa nguvu na ari zaidi ili kutimiza malengo waliojiwekea katika msimu huu.

“Habari za asubuhi Wananchi, asanteni kwa sapoti yenu ya jana. (juzi), tumewaangusha na inauma sana, imekuwa ngumu kuamka leo baada ya kupoteza dabi yangu ya kwanza lakini tunawahitaji mashabiki zetu sasa kuliko hapo awali.

“Tumejifunza kutokana na makosa yetu na tutarudi tukiwa na nguvu na njaa zaidi ya mafanikio,” amesema Musonda.

Yanga sc sasa iko kileleni kwa alama tano pekee kutoka nane za awali na ikitakiwa kushinda mechi mbili na sare moja katika michezo yake minne ijayo ya ligi kuu ili kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu kwa msimu wa huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala