Connect with us

Makala

Shikhalo Ajiunga na Kakamega Home Boys

Golikipa wa zamani wa Yanga SC , KMC na Mtibwa Sugar SC, Farouk Shikalo amejiunga na klabu ya Kakamega Homeboyz ya nchini Kenya.

Kipa huyo wa zamani wa timu hizo za nchini Tanzania pamoja na Bandari Fc ya nchini Kenya aliachana na Mtibwa Sugar kwa makubaliano ya pande mbili na kuamua kupumzika kwa muda mpaka aliposaini dili na timu hiyo ya nchini Kenya.

Shikhalo anakumbukwa hapa nchini kwa umahiri wake wa kuokoa michomo mikali kipindi akiwa katika ubora wake katika klabu ya Yanga sc na Bandari Fc lakini aliporomoka kiwango ghafka kiasi cha klabu ya Yanga sc kumtema na kujiunga na Kmc kisha Mtibwa Sugar ambapo alidumu kwa muda kisha kuvunja mkataba huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala