Connect with us

Makala

Simba sc Yaibuka Kibabe Kimataifa

Ndoto za klabu ya Simba sc kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kimataifa zimeanza kufufuka baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers Fc katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc licha ya kuanza vizuri kipindi cha kwanza iliwalazimu kusubiri mpaka mwishoni mwa kipindi hicho kupata bao pekee likifungwa na Cletous Chama kwa shuti kali na kufungua kufuri kali lililowekwa na walinzi wa Vipers Fc chini ya uongozi wa kipa Mudekereza aliyefanya kazi nzuri kuokoa hatari langoni.

Vipers nusura wasawazishe bao hilo mwanzoni kabisa mwa kipindi cha kwanza lakini kibendera cha mwamuzi wapembeni kilikua juu kuashiria kuwa ni mfungaji ameotea na kukataa bao hilo.

Pamoja na kufanikiwa kupata alama tatu bado Simba sc ipo chini hasa katika kushambulia kwa kasi pamoja na kuzuia wanaposhambuliwa hasa kwa kushtukiza.

Kutokana na ushindi huo sasa Simba sc imefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya pili ikiwa na alama sita katika msimamo wa kundi C huku Raja Casablanca wakiwa kileleni na alama 12 na Horoya wakiwa nafasi ya tatu na alama nne pekee huku Vipers wakishika mkia.

Mchezo unaofatia katika ya Simba sc na Horoya ndio utaamua hatma ya nani ataingia robo fainali na Raja Casablanca ambao kimsingi tayari wameshafuzu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala