Connect with us

Makala

Mastaa Mazembe Kukatwa Mishahara

Bosi wa klabu ya Tp Mazembe Moise Katumbi ameagiza mastaa wa klabu hiyo kukatwa mishahara yao kwa asilimia 25 endapo watashindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika wanayoshiriki hivi sasa.

Timu hiyo ipo katika kundi D la michuano hiyo ikiwa na klabu za Yanga sc,Us Monastry na Real Bamako ambapo katika msimamo wa kundi hilo inashika nafasi ya tatu huku Us Monastry na Yanga sc zikiwa juu katika michezo mitatu ya kila timu mpaka sasa ambapo katika mchezo ujao itawafuata Us Monastry ugenini.

Klabu hiyo inayonolewa na kocha Pampile Mihayo imekua na matokeo mabovu ikitoa ikiifunga Real Bamako na kukubali kufungwa na Yanga sc na Us Monastry katika uwanja wa nyumbani jijini Lubumbashi.

Bosi huyo ametoa uamuzi huo ili kuwafanya mastaa wa klabu hiyo wakina Mukoko Tonombe,Kinzubi na wengineo kukaza buti katika michezo mitatu iliyosalia ambapo watacheza miwili ugenini na mmoja dhidi ya Yanga sc nyumbani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala