Connect with us

Makala

Yanga sc Yahamia Chamazi Complex

Klabu ya Yanga sc sasa itatumia uwanja wa Chamazi Complex kama uwanja wa nyumbani katika mchezo wa kombe la shirikisho la AzamTv baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa katika matengenezo kwa muda.

Yanga sc itautumia uwanja huo unaomilikiwa na klabu ya Azam Fc katika mchezo wa siku ya ijumaa dhidi ya Tanzania Prisons mchezo wa hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho unaotarajiwa kuanza majira ya saa moja usiku.

Pamoja na hayo bado klabu ya Yanga sc itaendelea kuutumia uwanja wa Benjamini Mkapa kama uwanja wa nyumbani katika michuano ya kimataifa dhidi ya Real Bamako utakaofanyika siku ya Jumatano march 8.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala