Connect with us

Makala

Aziz Ki Aitwa B/Faso

Staa wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki ameitwa katika kikosi cha timu yake ya Taifa ya Burkina Faso kinachojiandaa na michezo miwili ya kimataifa yakalenda ya shirikisho la soka duniani (Fifa) dhidi ya Togo.

Aziz Ki aliyejiunga na klabu ya Yanga sc msimu huu alianza kwa kuchechemea katika ligi kuu nchini kutokana na kutozoea mazingira lakini kadri siku zinavyokwenda amefanikiwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu sambamba na kufunga magoli muhimu kwa klabu hiyo.

Moja ya mabao yatakayokumbukwa na mashabiki wa soka hasa nchini ni lile dhidi ya Club Africain nchini Tunisia ambapo aliunganisha kwa shuti kali pasi ya kichwa na Fiston Mayele na kuiwezesha Yanga sc kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Aziz Ki anatarajiwa kujiunga na timu yake ya taifa hivi karibuni baada ya kumaliza mechi za kombe la shirikisho na ile ya kimataifa dhidi ya Real Bamako inayotarajiwa kufanyika machi nane mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala