Connect with us

Makala

Try Again Aula Tena Simba sc

Mwenyekiti wa heshima wa klabu ya Simba sc na mfadhili wa klabu hiyo Mohamed Dewji amemchagua Salum Abdalah maarufu kama “Try Again” kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kwa mara ya pili baada ya muda wake kumalizika siku zilizopita.

Awali klabu hiyo ilifanya uchaguzi kuchagua viongozi wapya ambapo Murtaza Mangungu alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo kwa upande wa wanachama huku wajumbe kadhaa wakiongozwa na Asha Baraka wakichaguliwa katika uchaguzi huo uliokua na pilikapilika za kutosha.

Kwa upande wa Muwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji amemrejesha Try again kama Mwenyekiti wa klabu akimuwakilisha muwekezaji hiyo huku pia akiwafanyia tafrija fupi baadhi ya viongozi waliomaliza muda wao klabuni hapo hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wapya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala