Connect with us

Makala

Yanga sc Yatua Mali

Msafara wa wachezaji na viongozi wa klabu ya Yanga sc umefanikiwa kutua salama jijini Bamako nchini Mali kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Real Bamako ya nchini humo utakaofanyika siku ya Jumapili jioni.

Kikosi hicho kilivyotua nchini humo na moja kwa moja kuelekea hotelini ambapo masafara huo uliondoka Dar es salaam alfajiri ya Alhamis baada ya kumaliza kupata alama tatu dhidi ya Kmc katika mchezo wa ligi kuu nchini.

Yanga sc haikupata tabu baada ya kuingia nchini humo kutokana na uwepo wa wachezaji raia wa Mali katika kikosi hicho ambao ni Djigui Diarra na Mamadou Doumbia ambao nao ni maarufu nchini humo.

Yanga sc watafuta alama tatu baada ya kuifunga Tp mazembe kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika ambapo mpaka sasa wapo nafasi ya pili ya kundi hilo la D huku Real Bamako wakiwa nafasi ya mwisho ya msimamo wa kundi hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala