Connect with us

Makala

Yanga sc Yapoteza kwa Monastry

Klabu ya Yanga sc imepoteza mchezo wake wa kwanza wa kombe la shirikisho baada ya kufungwa kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika nchini Tunisia ikiwa na mchezo wa kwanza wa makundi kwa klabu hizo zilizo katika kundi D.

Yanga sc ilingia na mpango kazi wa kucheza mpira huku ikiamini itapata ushindi na kuwa na umiliki mkubwa wa mpira lakini kukosekana kwa umakini katika kuokoa mipira iliyokufa hasa kona na faulo ilisababisha Monastri kupata mabao mawili mapema zaidi dakika za 10 na 16 kupitia kwa Mohamed saghraoui na Boubacar Traore yote yakifungwa kwa kichwa.

Kutokana na kupoteza alama tatu Yanga sc ipo katika nafasi ya mwisho ya msimamo wa kundi D ambapo Tp Mazembe na Monastry wakiwa kileleni mwa msimamo huo ambapo wikiendi ijayo Yanga sc itawakaribisha Tp Mazembe katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala