Connect with us

Makala

Yanga sc Yaipiga 7-0 Rhino Rangers

Kwa mara ya pili klabu ya Yanga sc imefanikiwa kupata ushindi mnono baada ya ule dhidi ya Zalan Fc ambapo wameifunga timu ya Rhino Rangers ya mkoani Tabora kwa mabao 7-0 huku Kennedy Musonda akifanikiwa kufunga kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe.

Mvua ya magoli ilianzishwa na Dickson Ambundo dakika ya 7 kisha Kennedy Musonda alifunga mabao dakika za 16 na 46 huku Farid Mussa alifunga dakika ya 25 baada ya Aziz Ki kufunga dakika ya 20 huku Yannick Bangala nae akifunga dakika ya 26 na bao la mwisho la Yanga sc lilifungwa na David Bryson dakika ya 90+3.

Yanga sc baada ya ushindi huo sasa imefanikiwa kufuzu hatua inayofuatia ikiungana na timu nyingi za ligi kuu kufuzu huku ikitarajiwa kukutana na Tanzania Prisons katika hatua hiyo inayofuatia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala