Connect with us

Makala

Saido Kuikosa Simba sc

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Geita Gold Sc Saido Ntibanzokiza atakosekana katika michezo mitatu ya ligi kuu nchini baada ya kupata kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu kati ya klabu yake dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Nyakumbu mkoani Geita.

Saido ambaye katika mchezo huo alifunga bao la kwanza kwa klabu yake kwa penati dakika ya 34 huku pia akitoa assisti ya bao la pili kwa Juma Liuzio dakika ya 45 ya mchezo alipata kadi nyekundu dakika ya 67 ya mchezo baada ya kumchezea faulo mbaya Omar Sultani na mwamuzi kumzawadia kadi nyekundu huku Mtibwa wakisawazisha dakika ya 90 ya mchezo huo.

Kutokana na adhabu hiyo kiungo huyo tegemeo la Geita Gold sc ataikosa michezo miwili inayofuatia kati ya timu yake na klabu za Simba sc utakaofanyika Disemba 18 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza pamoja na ule wa Disemba 22 dhidi ya Azam Fc ambao nao utafanyika jijini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala