Connect with us

Makala

Wababe Wafuzu 16 Kombe la Dunia

Wababe wa soka barani Ulaya wameongoza mbio za kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini qatar baada ya mechi za raundi ya pili na tatu kwa baadhi ya makundi mbalimbali katika michuano hiyo.

Uingereza imekua katika ya timu za mwanzo kufuzu baada ya kuwa na matokeo mazuri ikifuatiwa na timu za mataifa ya Uholanzi,Ufaransa,Senegal,Poland,Marekani,Arjentina na Australia ambapo timu hizo zimekua na matokeo mazuri katika makundi ikilonganishwa na timu zingine.

Michuano ya hatua ya 16 bora inatarajiwa kuanza mapema baada ya makundi kumalizika ambapo kutakua na mtoano ambapo timu inapaswa kushinda mchezo husika na anayefungwa hutolewa katika mashindano hayo ambapo baada ya dakika 90 za mchezo zikimalizika bila mshindi kupoatikana basi zitaongezwa 30 ambapo ikiwa hakuna mshindi basi hatua ya mikwaju ya penati huamua mshindi.

Katika hatua hii hakuna droo bali kila washindi wa makundi husiku hukutana na washindi wa pili wa makundi husika kutokana na mpangilio wa makundi kwa herufi ambapo mshindi wa kwanza Kundi A atakutana na mshindi wa pili wa kundi B na kuendelea wakibadilishana kwa mfumo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala