Connect with us

Makala

Firmino Aachwa Kombe la Dunia

Staa wa timu ya taifa ya Brazil na mashambuliaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino ameachwa katika kikosi cha wachezaji 26 kilichotangazwa na kocha wa timu hiyo Tite alitaja mastaa mbalimbali hasa wanaosakata soka barani ulaya na jina la staa huyo halikuwamo hivyo kuzua gumzo miongoni mwa wadau wa soka Duniani.

Moja ya hoja kubwa ni kitendo cha kocha Tite kumuacha Firmino mwenye mwendelezo mzuri tangu msimu uliopita na kumchukua staa wa Arsenal Gabriel Martinelli mwenye mechi tatu pekee za timu ya Taifa huku akiwaita pia washambuliaji Richarlison na kinda wa klabu ya Manchester United Anton pamoja na Gabriel Jesus wa Arsenal.

Tite pia ameita karibia mastaa wote wa eneo la kiungo wanaocheza ligi kuu ya Uingereza akiwajumuisha Fred na Casemiro kutoka Man utd na Bruno Guimaraes wa Newcastle United, Fabinho wa Liverpool na Lucas Paqueta wa Newcastle United.

Firmino licha ya kushiriki katika mechi za kukata tiketi za kushiriki fainali hizo ameachwa pamoja na wachezaji wengine wanne ambao ni beki wa pembeni wa  Nottingham Forest  Renan Lodi, beki wa As Roma Roban Ibanez na staa wa Atletico Madrid Matheus Cunha.

Goalkeepers: Alisson (Liverpool), Ederson (Manchester City), Weverton (Palmeiras)

Defenders: Dani Alves (Pumas UNAM), Danilo (Juventus), Alex Sandro (Juventus), Alex Telles (Sevilla), Bremer (Juventus), Eder Militao (Real Madrid), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Thiago Silva (Chelsea)

Midfielders: Bruno Guimaraes (Newcastle), Casemiro (Manchester United), Everton Ribeiro (Flamengo), Fabinho (Liverpool), Fred (Manchester United), Lucas Paqueta (West Ham)

Attackers: Antony (Manchester United), Gabriel Jesus (Arsenal), Gabriel Martinelli (Arsenal), Neymar (Paris Saint-Germain), Pedro (Flamengo), Raphinha (Barcelona), Richarlison (Tottenham), Rodrygo (Real Madrid), Vinicius Jr (Real Madrid)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala