Connect with us

Makala

Yanga sc Yatupiwa Waarabu Caf

Klabu ya Yanga sc imepangwa kucheza na waarabu wa Club Africains katika hatua ya mchujo ili kufuzu michuano ya kombe la shirikisho baada ya kutolewa na klabu ya Al Hilal na kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Katika Droo hiyo iliyochezeshwa mapema jana mchana Yanga sc itacheza mchezo wa kwanza hapa jijini Dar es salaam Novemba 2 katika uwanja wa Benjamini Mkapa huku marudiano yakipangwa kufanyika Novemba 9 huko nchini Tunisia.

Yanga sc wanapaswa kuhakikisha hawarudii makosa katika mchezo wa mwanzo hapa nchini kwani watakua na kibarua kizito ugenini ambapo klabu hiyo imekua na utamuduni wa kutofungika ikiwa uwanja wa nyumbani ambapo katika mchezo wa mwisho iliwafunga Kipanga Fc ya Zanzibar kwa bao 7-0 na kufanikiwa kufuzu hatua ya pili ya mtoano.

Club Afrcains ni moja ya timu kongwe nchini Tunisia ikiwa imeanzishwa mwaka 1920 ambapo imefanikiwa kuchukua mataji ya ligi kuu nchini humo mara 13 na kombe la ligi mara 13 huku ikimaliza katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu nchini humo msimu uliopita.Droo kamili ya kombe la shirikisho ni kama ifuatavyo:

Rail Kadiogo (BUR) or V Club (COD) v St Eloi Lupopo (COD)

Royal Leopard (ESW) v Real Bamako (MLI)

TP Mazembe (COD) v Royal AM (RSA)

Primeiro Agosto (ANG) v Future (EGY)

ASEC Mimosas (CIV) v SC Gagnoa (CIV)

Djoliba (MLI) v FAR Rabat (MAR)

Al Ahly Tripoli (LBA) v Marumo Gallants (RSA)

ASKO Kara (TOG) v CS Sfaxien (TUN)

Young Africans (TAN) v Club Africain (TUN)

Flambeau Centre (BDI) v DC Motema Pembe (COD)

Rivers Utd (NGR) v Al Nasr (LBA)

US Monastir (TUN) v Renaissance Berkane (MAR, holders)

Cape Town City (RSA) v USM Alger (ALG)

Nigelec (NIG) v Pyramids (EGY)

La Passe (SEY) v Diables Noirs (CGO)

Plateau Utd (NGR) v Al Akhdar (LBA)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala