Connect with us

Makala

Benzema Atwaa Ballon D’or

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema ameibuka kinara na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia(Ballon D’or) inayolewa na shirikisho la soka Duniani Fifa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi maarufu wa Théâtre du Châtelet uliopo jijini Paris Ufaransa.

Katika Hafla hiyo Benzema amewashinda Robert Lewandowski, Sadio Mane na Kevin De Bruyne huku akiweka rekodi ya kuwa mfaransa wa pili kuchukua tuzo hiyo baada ya Zinedine Zidane aliyechukua mwaka 1998 huku ushindi wake ukichagizwa na kuwa na msimu mzuri katika klabu yake ya Real Madrid huku pia akiweka rekodi ya kutwa tuzo hiyo akiwa na umri mkubwa wa miaka 34 tangu alivyofanya hivyo Stanley Matthews mwaka 1956.

“Ninajivunia sana na ni kazi nyingi zimefanyika ikiwa ni ndoto ya kila mtoto” Alisema Benzema akipokea tuzo hiyo siku ya Jumatatu usiku katika hafla ambayo ilijaa mastaa wa soka duniani.

“Nilikua na vipindi vigumu hasa baada ya kutochaguliwa katika timu ya Taifa na sikukata tamaa”Alisema Benzema akikabidhiwa tuzo hiyo na kocha wake wa zamani katika klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane.

Ushindi huo kwa Benzema unakuja baada ya kuwa na msimu mzuri katika klabu ya Real Madrid akifunga jumla ya mabao 44 katika michezo 46 huku magoli yake 15 katika ligi ya mabingwa barani ulaya yakiisaidia Real Madrid kutwa taji la 14 la Ulaya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala