Connect with us

Makala

Kamwe,Priva Wakiwasha Yanga sc

Waandishi wa habari Ally Kamwe na Priva Shayo wameanza cheche siku chache baada ya kutambulishwa kama watendaji wapya wa klabu ya Yanga sc katika nafasi za Afisa Habari na msimamizi wa maudhui wa klabu hiyo ambapo kwa nyakati tofauti tofauti wameonyesha jinsi gani mashabiki wa klabu hiyo walivyopakua applikesheni ya klabu hiyo pamoja na kutembelea website mpya.

Priva ambaye amejiunga na Yanga sc akitokea kituo cha redio cha Clouds Fm alipokua kama mchambuzi wa habari za michezo na amekwenda Yanga sc ambapo atakua msimamizi wa maudhui ya mitandaoni huku Ally Kamwe yeye ameenda klabuni hapo kama Afisa Habari akitokea Azam Tv alipokua mchambuzi wa masuala ya soka.

Yanga sc wameajiri watendaji wapya na kutambulisha pamoja na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine aliyechukua nafasi ya Senzo Mazingiza huku Kamwe akichukua nafasi ya Hassan Bumbuli na nafasi ya Priva ikiwa ni nafasi mpya klabuni hapo.

Kamwe mapema hivi leo alikua katika mahojiano na kituo cha redio cha Wasafi ambapo alizungumza mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo hasa mchezo unafuata dhidi ya Al Hilal utakaofanyika siku jumamosi oktoba 8.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala