Klabu ya Simba sc imempa mkoni wa kwaheri winga Benard Morrison kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake cha hivi karibuni huku nidhamu ikichangia kufikia maamuzi hayo.
Winga huyo alisajiliwa kwa mbwembwe akitokea klabu ya Yanga sc huku usajili huo ukileta utata kiasi cha klabu ya Yanga sc kuamua kukimbilia mahakama ya kimataifa ya masuala ya soka (Cas) ili kutafuta haki yao lakini kesi hiyo mchezaji huyo alishinda na Yanga sc kumkosa.
Morrison licha ya kuwa na kiwango kikubwa inatajwa masihara kazini ikiwemo kuchagua mechi za kufanya vizuri imemfanya mwalimu Pablo Franco kuagiza uongozi kuachana nae huku utovu wa nidhamu uliokithiri ikisemekana mpaka kutoroka kambini na tukio la juzi kupigana na mashabiki katika mchezo dhidi ya Yanga sc ni moja ya mambo yaliyowalazimisha Simba sc kuchukua hatua hiyo ili kulinda hadhi na thamani ya kikosi katika suala zima la maadili kazini.
Simba sc imemalizana kisomi na Morrison baada ya kukubali kumlipa stahiki zake zote ikiwemo mishahara ya miezi iliyobakia pamoja na kumpa mapumziko mpaka mkataba wake utakapoisha huku ikimtakia kila la kheri katika timu atakayojiunga nayo hapo baadae hukunae staa huyo akisema kuwa majukumu ya kifamilia ndio sababu kuu ya kupewa mapumziko hayo japo taarifa za ndani ni kwamba pande zote zilikubaliana kusema hivyo ili kulinda heshima ya pande zote mbili.
Pamoja na klabu hiyo kumtema mchezaji huyo kumekua na taarifa kuwa anavivutia vvilabu vya Yanga sc na Azam fc ambao wanahisi bado winga huyo anawafaa kupigania ubingwa msimu ujao.