Connect with us

Soka

Zahera Aula Congo Drc

Aliyekua kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc Mwinyi Zahera amechaguliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo Drc akimsadia kocha raia wa Argentina  Hector Cuper baada ya shirikisho la soka nchini humo kumchagua kushikiria nafasi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo imesema kuwa Zahera ameteuliwa baada ya kocha msaidizi wa timu hiyo Daouda Lupembe kupata kazi ya kuifundisha timu ya ligi kuu nchini humo ya Sanga Balende.

Zahera anateuliwa kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine baada ya hapo awali kuwa kocha msaidizi huku akiifundisha klabu ya Yanga sc na hivi sasa alikua ni mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Yanga sc anayehusika zaidi na kunoa vijana wa klabu hiyo.

‘Nimepokea taarifa na ni heshima kwangu kurudi kuifundisha timu ya Taifa kumsaidia kocha mkuu lakini jambo kubwa ni kupata nguvu baada ya kukosa kufuzu kwenda kombe la dunia nchini qatar’ Alisema kocha Zahera.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka