Connect with us

Soka

Saido,Yacouba Kuwakosa Namungo Fc

Pamoja na kwamba amebakisha chini ya siku arobaini amalize mkataba wake na klabu ya Yanga sc mchezaji Saido Ntibanzokiza ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Mchezaji huyo ameibuka kuwa mmoja ya wachezaji muhimu katika klabu yake akifunga mabao 6 nyuma ya kinara Fiston Mayele amekua akisumbuliwa na majeraha madogo madogo yanayomfanya akose baadhi ya michezo ikiwemo huu dhidi ya Namungo Fc ambao Yanga sc wanahitaji alama tatu muhimu.

Yanga sc wakishinda mchezo huo wataongeza pengo la alama mpaka 13 dhidi ya hasimu wake Simba sc kutoka kumi za hivi sasa huku wakijiandaa kuvaana wao kwa wao April 30.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka