Connect with us

Makala

Makapu Atoweka Polisi Tanzania

Mchezaji wa klabu ya Polisi Tanzania Said Juma Makapu haonekani katika klabu hiyo tangu alipoondoka siku moja kabla ya mchezo wa ligi kuu baina ya klabu hiyo na Simba sc Klabu uliofanyika katika uwanja wa ushirika mjini Moshi.

Makapu hakuonekana katika mchezo huo ulioisha kwa sare na kusababisha Simba sc kuachwa alama 10 na watani wa jadi Yanga sc huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kwa mujibu wa viongozi wa klabu hiyo mpaka sasa hawajui mchezaji huyo mahali alipo huku akiwa hapokei simu na wakati mwingine hapatikani kabisa japo anahitajika kuwa klabuni kwa mwajiri wake.

Msemaji wa klabu hiyo inayomilikiwa na jeshi la Polisi nchini Frank Lukwaro amesema bado wanaendelea kumtafuta mchezaji huyo ili kujua zaidi sababu za kutoweka kambini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala