Connect with us

Makala

Yanga sc Yatinga Nusu Fainali Shirikisho

Licha ya mshambuliaji Fiston Mayele kushindwa kutetema katika mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa bado klabu ya Yanga sc ilifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Geita Gold Sports 1-1 (7-6 Penati).

Katika mchezo Geita Gold Sports inayofundishwa na kocha Mtanzania Felix Minziro ilimiliki mpira na kutoa upinzani kwa Yanga sc huku wakifanikiwa kumpoteza kabisa mshambuliaji Fiston Mayele katika dakika zote tisini za mchezo ambao Yanga sc iliwakosa viungo Abubakary Salum,Feisal Salum na Khalid Aucho ambao wana majeraha.

Mpaka kipindi cha kwanza matokeo yalikua bila bila ambapo kuingia kwa mshambuliaji Hoffem Chikola kulileta mabadiliko makubwa kwa upande wa Geita Gold na kuwafanya wapate bao la utangulizi dakika ya 88 likifungwa na Hoffem ambaye aligongeana vizuri na George Mpole na Juma Mahadhi bao ambalo kinyume na matarajio ya wengi lilisawazishwa kwa penati na Djuma Shabani dakika ya 90+3.

Hatua ya mikwaju ya penati iliwadia ambapo Yanga sc ilifanikiwa kufunga kupitia kwa Yannick Bangala,Jesus Moloko,Saido Ntibanzokiza,Bakari Mwamnyeto,Djuma Shabani,Fiston Mayele na Dickson Job huku kwa upande wa Geita Gold sc waliopata ni Duchu, George Mpole, Maka Edward ambaye alikosa, Adeyum Saleh, Chikola, Kelvin Yondani, Juma Mahadhi ambaye alikosa pia.

Yanga sc sasa itavaana na mshindi kati ya Simba sc dhidi ya Pamba sc katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo ambalo mshindi atajikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barabi Afrika.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala