Connect with us

Makala

Azam Yaipumzikia Yanga sc

Kocha wa klabu ya Azam Fc Abdihimid Moallin ametoa mapumziko ya siku kadhaa kwa mastaa wa timu yake ili kukusanya nguvu kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya klabu ya Yanga sc utakaofanyika Aprili 6 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo ametoa mapumziko hayo baada ya timu yake kuichapa timu ya taifa ya Somalia kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi huku nyavu za Somalia zikitikiswa na Ayoub Lyanga,Shabani Idd na Idris Mbombo ambapo kocha Moallin aliwapa mapumziko wachezaji wake ili wakirejea wawe tayari kwa ajili ya mazoezi ya nguvu kuikabili Yanga sc.

Azam Fc ni timu ya mwisho kuifunga Yanga sc katika michezo ya ligi kuu nchini ambapo walipokutana mwaka jana Yanga sc ililala kwa bao 1 lililofungwa na Prince Dube huku kwa upande wa ligi kuu msimu huu Yanga sc ilishinda kwa mabao 2-0.

Azam Fc imekua na mwenendo wa kusuasua katika ligi kuu nchini msimu huu ambapo imecheza jumla ya michezo 18 ikiwa na alama 28 ikiachwa alama 20 na Yanga sc ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala