Connect with us

Makala

Kagoma Azigonganisha Simba sc na Yanga sc

Kiungo wa ulinzi wa klabu ya Singida Fountain Gate Yussuph Kagoma amezigonganisha klabu za Simba sc na Yanga sc kutokana na klabu zote mbili kudaiwa kumalizana mchezaji huyo kwa kumsainisha mikataba ya miaka miwili kila mmoja.

Yanga sc walikua wa kwanza kumalizana na Kagoma ambapo walinunua mkataba wake wa mwaka mmoja aliokua nao katika klabu yake ya Singida Fountain Gate ambao alikua na mgogoro nao hali iliyomfanya aondoke kwenye kambi ya timu hiyo akiwa na mkataba ambao Yanga sc wameununua na kumalizana na mchezaji huyo akisubiri kutambulishwa tu.

Wakati hayo yakimalizika mchezaji huyo alifuatwa na viongozi wa klabu ya Simba sc waliokua wanahitaji kumsajili na inasemekana mchezaji huyo alikubali ofa ya Simba sc ambayo ni kubwa kuliko ya Yanga sc japo tayari alishasaini Yanga sc.

Simba sc baada ya kumshawishi mchezaji huyo walihamia kwa klabu ya Singida Fountain Gate kuununua mkataba wa mchezaji huyo hali iliyowashtua viongozi wa Singida Fountain Gate kwa maana tayari walishamalizana na Yanga sc kuhusu mchezaji huyo.

Mpaka sasa asilimia kubwa ni Kagoma kuichezea Yanga sc ambayo ilikamilisha kila kitu kuhusu usajili wake mapema kabisa huku mchezaji akilipwa na dau la usajili ambapo licha ya mchezaji huyo kuvutiwa na ofa kubwa ya klabu ya Simba sc yenye mshahara mnono na hela ya kusainia dili hilo.

Simba sc ipo kwenye maboresho makubwa ya kikosi chake ikipanga kuwatema mastaa kadhaa na kusajili vijana wapya wenye chachu ya mafanikio na wanamuona Kagoma kama mbadala sahihi ya Mzamiru Yassin ambaye amekua na kazi kubwa ya kufanya bila kuwa na mbadala sahihi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala