Connect with us

Makala

Man United Mabingwa Carabao Cup

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuwa mabingwa wa kombe la Carabao Cup baada ya kuifunga klabu ya Newcastle United kwa maba0 2-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza mapema jioni ya Jumapili February 26.

Ushindi huo unaifanya Man United kumaliza ukame wa miaka sita bila kombe ambapo matumaini ya kupata kombe hilo yalianza mapema dakika ya 33 baada ya Casemiro kufunga bao zuri la kichwa huku dakika sita baadae Sven Botman alijifunga bao kutokana na Marcus Rashford kumlazimisha kufanya makosa hayo.

Aaron Wan-Bisaka alionyesha mchezo mzuri hasa kipindi cha pili na kufanikiwa kuzima mashambulizi mengi ya Newcastle huku pia akiwashangaza wengi kwa kiwango hicho kutokana na kutokuwemo katika mipango ya kocha Erick Ten Hag hasa mwanzoni mwa msimu huu.

 “Ni nidhamu nzuri kwa mara nyingine ya kupigana na kujitoa kwa kila kitu japo kila siku sio mchezo mzuri lakini ulikua mchezo imara kwetu”.

“Cha kwanza ni kushinda taji la kwanza na hicho ndicho tulichofanya leo kisha unaweza kupata hamasa kutoka hapo na kujiamini kuwa tunaweza kufanya hicho kitu”.

Imewachukua takribani miaka sita tangu 2016 kwa klabu ya Manchester United kuweza kushindi kombe baada ya kuwa na ukame huku wakiwa na viwango vya chini uwanjani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala