Connect with us

Makala

Lampard Atua Everton

Klabu ya Everton imemteua mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Frank Lampard kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo tayari kocha huyo amejiunga na benchi la ufundi la klabu hiyo kuanza kazi mara moja baada ya uteuzi akirithi mkongwe Rafa Benitez.

Mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri alikutana na watahiniwa watatu wa nafasi hiyo ambapo Lampard alikua ni mmoja wapo huku wengine wakiwa ni Vitor Pereira na aliyekua ameshikilia nafasi hiyo kwa muda Duncan Ferguson ambaye yeye alisisitiza kuwa anahitaji nafasi hiyo iliyokaliwa na Rafa Benitez kwa muda wa miezi saba kwa udi na uvumba.

“Nimefurahishwa sana na Frank kujiunga nasi,ni kijana mdogo anayevutia nadani na nje ya uwanja huku akiwa amecheza soka katika levo za juu hivyo mpira upo damuni”Alisema bosi na mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri.

“Ametufurahisha sana kipindi cha usaili na tuko tayari kumpa sapoti yetu sote katika kipindi hiki maana atasaidia kuibust timu kwa haraka zaidi”Alisisitiza bosi huyo mkubwa na mwenye nguvu klabu hapo.

Pia Lampard tayari amemuomba aliyekua kocha wa muda wa klabu hiyo Duncan Ferguson kusalia klabuni hapo amsaidie katika benchi la ufundi huku kocha wa zamani wa Swansea na Derby Country Paul Lambart akichaguliwa kuwa kocha wa kikosi cha kwanza.

Lampard hakua na ajira tangu mwezi januari alipotimuliwa katika klabu ya Chelsea kutokana na matokeo mabovu ambapo alikaa klabuni hapo kwa takribani miezi kumi na nane akiicha timu hiyo katika nafasi ya tisa ya msimamo huku akifanikiwa kuifikisha timu fainali ya kombe la FA na kuingiza katika nafasi za nne za juu katika ligi kuu nchini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala