Connect with us

Soka

Stars yamaliza wa tatu kundi J

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imelazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Madagascar mjini Atarsntananarivo na kumaliza wakiwa wa tatu katika msimamo wa kundi J kufuzu kombe la dunia Qatar 2022.

Stars ilianza kupata goli dakika ya 25 kupitia kwa mshambuliaji wa Wydad Casablanca Simon Msuva akimalizia pasi nzuri kutoka kwa kiungo wa Yanga Feisal Salum,kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 74 kupitia kwa mshambuliaji wao wa kati Hakim Abdallah akitumia vizuri makosa ya mabeki kushindwa kuundoa kwenye hatari mpira wa adhabu.

Katika mchezo huyo Tanzania ilimkosa nahodha wake Mbwana Samatta,beki wa kati Bakari Nondo na mlinda mlando Aishi Manula kutokana na kudaiwa kuwa na maambukizi ya UVIKO-19.

Mchezo mwingine wa kundi hilo umeshuhudia DR Congo wakikata tiketi ya kumi 10 ambapo timu hizo zitamenyana kupata wawakilishi  5 kutoka Afrika kwenda michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwakani nchi Qatar.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka