Connect with us

Soka

CEO Dortmund aiponda Man Utd kisa Sancho

Mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Joachim Watzke amesema kuwa anashangazwa na jinsi kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pamoja na uongozi mzima wa timu hiyo kwa jinsi wanavyomtendea Jadon Sancho.

Samcho aliyefanya vizuri kipindi alipokuwa Dortmund ameanza kwa kusuasua ndani ya Man Utd ikiwa ni pamoja na kuanza michezo miwili tu kati ya michezo nane ya timu hiyo msimu huu kiasi cha kupoteza hali ya kujiamini kwa mchezaji huyo.

Watzke amesikitishwa pia na kitendo cha mchezaji wa timu hiyo kutokupewa umuhimu katika timu ya taifa ya Uingereza hasa kwenye michuano ya Euro 2020.

Mtendaji huyo amesema ”inaumiza kuona Sancho hapewi umuhimu mkubwa na Ole pamoja na Southgate,nampenda Sancho ukimuona anavyocheza unaweza tokwa na machozi”.

Mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa alitarajiwa kuwa msaada mkubwa ndani ya Man Utd alipojiunga nayo msimu huu akitokea Dortmund kwa dau la Euro milioni 73,lakini mambo yamekuwa tofauti na pengine ubaguzi wa rangi aliofanuiwa katika fainali ya Euro 2020 kwa kukosa penati imemuathiri kisaikolojia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka