Connect with us

Makala

Chama Asimamishwa Simba sc

Uongozi wa klabu ya Simba sc umetangaza kumsimamisha kiungo Cletous Chama pamoja na Nassoro Kapama kwa tuhuma za utovu wa nidhamu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo kwa umma.

Taarifa kutoka ndani zaidi zinasema kuwa Chama amekua na kawaida ya kuchelewa kufika mazoezini huku pia akidaiwa kumfokea mmoja ya makocha wasaidizi wa klabu hiyo huku Mwalimu Benchika akipitiza panga hilo ikiwa ni moja ya njia za kutengeneza nidhamu klabuni humo.

Pamoja na staa huyo kufungiwa pia baadhi ya mastaa kikosini humo wamekatwa mishahara kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu huku Kapama akisimamishwa kutokana na kuripoti kuwa anaumwa lakini hakufika kambini ili kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa klabu hiyo kwa matibabu zaidi.

Baadhi wa wadau wa soka nchini wamekua na maoni tofauti kuhusu kusimamishwa kwa mastaa hao hasa Chama ambapo baadhi wanasimama na msimamo wa klabu huku wengine wakiona huo ndio mwisho wa staa huyo klabuni hapo kutokana na kuwa na mfululizo wa makosa.

“Kwanza Chama siku zote utasikia anaidai Simba na ni mchezaji anayesajiliwa na timu nyingine kila usajili(wakati wa usajili lazima utasikia Chama anasajiliwa na timu fulani)”

“Amekuja Robertinho na akaonekana ana taratibu zake lakini baada ya kumfanyia sub watu walilaumu sana ,Robertinho akakaubali kuingia kwenye mfumo wa Chama”

“Robertinho ameondoka kaja huyu Benchikha ambaye amesema hapana lazima aingie kwenye mfumo ama zake ama zangu”.Alisema Mwandishi wa habari Master Tindwa kutoka Clouds Fc.

“Ni mapema sana kufikiria huo mwisho wa Chama kwa huku kusimamishwa ,mimi ninachokiona Klabu na mchezaji kutokea changamoto ni kawaida ,imekuwa stori kubwa kwa sababu ni Chama”Alisema Mwandishi wa Clouds Fc Yahaya Njenge.

“Hata ukienda ukatafiti kwenye NBC wachezaji waliosimamishwa sio Chama peke yake,hata kwenye hii taarifa ni Chama na Kapama. Kibaya zaidi hakuna ufafanuzi kuwa huo utovu wa nidhamu ni upi ?”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala