Connect with us

Makala

Manara Amkataaa Barbara

Afisa mhamasishaji wa klabu ya Yanga sc Haji Manara amekataa kumpongeza mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc ambaye ameteuliwa na shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kuwa mjumbe kwenye kamati ya mashindano ya shirikisho hilo barani Afrika.

Katika uteuzi huo uliotangazwa jana na shirikisho hilo umezua mjadala kwa wadau wa soka nchini hasa vyombo vya habari huku watu mbalimbali wakimpongeza likiwemo shirikisho la soka nchini (Tff).

Hali imekua taofauti kwa Afisa huyo ambaye amekataa kumpongeza wakati alipoulizwa na moja wa watangaza Loveness Banzi katika kipindi cha usiku cha Redio ya Wasafi Fm.

“ Kwa siasa za mpira wa Tanzania siwezi kumpongeza Barbara hata kidogo kwasababu hata sisi tunafanya mambo makubwa na hatujawahi kupongezwa hatuna utamaduni huo”Alisema Haji Manara.

Tangu wawili hao waingie kwenye mgogoro baada ya Haji kushutumiwa kuwa anaihujumu klabu ya Simba sc ambapo aliachia ngazi na kujiunga na klabu ya Yanga sc wamekua hawana mahusiano mazuri huku Manara akimpiga vijembe mara kwa mara bosi huyo mwanamama pekee katika soka nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala