Connect with us

Soka

Simba Sc Vs Azam Fc Kufanyika Ccm Kirumba

Klabu ya Simba sc imeuhamishia mchezo wa kiporo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza ambapo unatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa februari 9 mwaka huu.

Awali mchezo huo ulikua ufanyike katika uwanja wa Benjamini Mkapa mwishoni mwa mwaka jana lakini ulisogezwa mbele kupisha maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambapo baadhi ya mastaa wa timu hiyo walikua wanashiriki kupitia mataifa yao.

Simba sc wanalazimika kuupeleka mchezo huo jijini Mwanza kutokana na uwanja wa Benjamini Mkapa kuzuiwa kutumika na Serikali kutokana na kuwa katika ukarabati mkubwa hivyo kuruhusu mechi za kimataifa pekee kufanyika hapo kwa sasa huku ombi lao la kutumia uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar likiwa na kizungumkuti cha kanuni.

Simba sc inalazimika kushinda mchezo huo ili kujiongezea uhakika ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu ilioukosa kwa misimu miwili mfululizo ukibebwa na Yanga sc ambapo pia katika msimamo klabu hiyo iko nafasi ya tatu mpaka sasa ikiwa na alama 26 katika michezo 11 huku Azam Fc ikiwa nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 31 na Yanga sc ikiwa kileleni na alama 32.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka