Connect with us

Soka

Zanzibar queens Wala 5

Timu ya taifa ya wanawake ya Zanzibar Queens wamefungwa jumla ya magoli 5-0 na timu ya taifa ya Sudan kusini katika michuano ya Cecafa kwa wanawake inayoendelea nchini.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa chamazi ulimalizika kwa simanzi kwa watanzania walioshuhudia mchezo huo baada ya kiwango duni cha timu hiyo ambayo mechi ya kwanza ilifungwa kwa idadi kama hiyo ya magoli na Burundi.

Awali kabla ya mchezo huo kocha wa timu hiyo Mohamed Salaa alisema timu hiyo ilianza vibaya michuano hiyo kutokana na ukata ambapo wachezaji hawajalipwa posho kama ilivyo kwa timu nyingine.

“Sisi hatujapewa kitu chochote kuanzia posho za wachezaji mpaka jezi za kuvaa tumeshindwa hata kuweka timu kambini kutokana na ukata tuliokua nao”.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka