Connect with us

Soka

Zahera Atua,Kuwaona Balinya,Sibomana Moro

Hatimaye kocha mkuu wa Yanga sc Mwinyi Zahera ametua nchini leo alfajiri akitokea nchini Ufaransa alipokua na mapumziko baada ya kutoka katika michuano ya Afcon na timu ya taifa ya Kongo.

Zahera ametua nchini saa 12 na dakika 4 asubuhi ya leo kwa ndege ya shirika la Rwanda(Rwanda Air) na moja kwa moja ataunganisha kambini Morogoro kuungana na timu iliyopo kambini na atashuhudia mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Eagle Noir ya nchini Burundi mchezo utakaochezwa katika chuo cha biblia mkoani humo.

Zahera alipewa likizo ya wiki mbili kuanzia tarehe 13 mwezi wa saba nakurejea kwake kumezima tetesi zilizosambaa za kuwa amegoma kushinikiza kulipwa madai yake ya fedha kitu ambacho kocha huyo alikanusha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka