Connect with us

Soka

Zahera Atimuliwa Yanga

Klabu ya Yanga sc imeachana na kocha Mwinyi Zahera baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha uwanjani licha ya usajili kabambe ambao ulifanyika msimu huu kwa mapendekezo ya kocha huyo.

Zahera alijiunga na Yanga sc msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili japo aliendelea na nafasi yake ya ukocha msaidizi wa timu ya taifa ya Kongo hivyo kufanya timu hiyo kumtegemea kocha msaidizi Noel Mwandila pindi anapokua na majukumu ya timu ya taifa.

Yanga imeamua kuachana na Zahera na benchi zima la ufundi la klabu hiyo wakiwemo wasaidizi wake ,meneja na kocha wa makipa na imemtea kocha Bonifasi Mkwasa kushika nafasi hiyo huku ikidaiwa watamteua kocha wa Bandari fc Ben Mwalala kuchukua nafasi ya Zahera.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka