Connect with us

Soka

Zahera Arejea Kufuata Manoti

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Kongo Mwinyi Zahera amerejea nchini kufuatilia stahiki zake katika klabu ya Yanga baada ya timu hiyo kuvunja mkataba na kocha huyo.

Zahera alivunjiwa mkataba na klabu hiyo ukiwa umebakiza zaidi ya miezi sita ili kufikia tamati baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha katika klabu hiyo.

Kocha huyo baada ya kuvunjiwa mkataba aliondoka nchini kujiunga na timu ya taifa na baada ya kumaliza majukumu amerejea nchini ili kuchukua stahiki zake ambazo ni zaidi ya shilingi milioni hamsini za kitanzania ikiwa ni majumuisho ya pesa ya kuvunjia mkataba na madeni ya mishahara iliyopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka