Connect with us

Soka

Zahera Aipa Ushindi Yanga

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc Mwinyi Zahera ameipa ushindi klabu ya Yanga sc katika mchezo wa jumapili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho ambao utazikutanisha Simba na Yanga.

Zahera anayeishi nchini kwa sasa alisema hayo wakati akihojiwa na gazeti la championi ambapo alisema kuwa “Yanga wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo wa nusu fainali kwa sababu kiufundi wamekuwa na hamasa kubwa ya kushinda katika mechi dhidi ya Simba, sasa wanachotaka ni kuendeleza pale walipoishia, japokuwa watu wanasema Simba watashinda ila kwangu mimi ni tofauti.

“Unajua ukiachana na wachezaji wa Yanga lakini uongozi wa GSM wanajua kuandaa timu vizuri katika mechi na Simba sasa lazima wahakikishe wanapata matokeo kwa kuwa ndiyo njia pekee ya wao kupata nafasi ya kucheza fainali, ikiwezekana ubingwa wa kwenda kimataifa, hivyo naamini Yanga watashinda bila tatizo mchezo huo.

“Simba tayari ni bingwa kwa sasa hana cha kupoteza tofauti na Yanga ambao wanahitaji zaidi ushindi hivyo utakuwa ni mchezo mzuri na wenye ushindani mkubwa,” amesema.

Mshindi katika mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Namungo na Sahale all Stars kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka