Connect with us

Soka

Yanga,La Liga Kimeeleweka

Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya La liga inayosimamia ligi kuu ya nchini Hispania jana jijini Dar es salaam kuelekea mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dk.Mshindo Msolla na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya Gsm Eng.Hersi Said wakisaini Mkataba wa Ushirikiano na Kampuni ya La liga jana jijini Dar es salaam.

Mkataba huo utajumuisha klabu  hiyo na kampuni hiyo ya La liga huku kampuni ya Gsm ikiwa kama mlipaji mkuu wa gharama hizo zinazokadiliwa kufika shilingi bilioni 2 ambapo zitalipwa kwa awamu nne.

Pia katika mkataba klabu hiyo itashirikiana na klabu ya Sevila inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania katika mambo mbalimbali ya kiufundi,utendaji pamoja na kusaka vipaji na kuviendeleza.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz alisema kuwa katika mabadiliko hayo idara ya kwanza kuathirika ni idara ya utawala pamoja na ushirikishaji wanachama(Fans Engagement).

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikua Rais Mstaafu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Naibu Waziri wa Ajira,kazi na vijana Mhe.Anthony Mavunde huku pia Wallace Karia Rais wa shirikisho la soka nchini pia alikuwepo sambamba na watu maarufu mbalimbali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka