Connect with us

Soka

Yanga Yaweka Rekodi Taifa

Mechi ya watani wa jadi Yanga vs Simba iliyochezwa Jumapili Machi 8, 2020 imevunja rekodi ya mapato kwa kuiingizia serikali shilingi milioni 153.2 kiasi ambacho hakijawahi kupatikana katika historia ya mechi za watani hao.

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas wakati akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma.

Aidha ukiondoa mapato ya Serikali, jumla ya Tsh Milioni 545.4 zilikuwa ni mapato ya timu (Yanga) ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo uliofanyika machi 8 mwaka huu.

Hii ni rekodi mpya katika historia ya uwanja huo uliozinduliwa mwaka 2007 ukilinganisha na mechi zingine zilizochezwa uwanja hapo zikiwemo za kimataifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka