Connect with us

Soka

Yanga yatupwa nje Mapinduzi cup

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Yanga sc imeyaaga mashindano hayo baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo hii leo dhidi ya Azam fc.

Changamoto ya mikwaju ya penati ndio imewatoa wananchi baada ya Azam kupata penati zake zote huku wao wakikosa mmoja uliopigwa na beki wa kushoto Yasin Mustapha alyeupaisha juu ya lango.

Dakika tisini za mchezo zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana na ndipo kanuni ya michuano hiyo ya kupigwa kwa penati baada ya dakika tisini ilipofuatwa na mwamuzi wa mchezo huo.

Ikiwa imebaki dakika moja kati ya tatu za nyongeza mpira kumalizika kocha wa Yanga Cedric Kaze alimtoa mlinda mlango Aboutwalib Mshery na kumuingiza Eric Johora hata hivyo hakuweza kuibeba timu yake baada ya kufungwa penati zote tisa.Kila timu ilipata penati tano za mwanzo na ndipo walipoingia zile za ziada ambapo Azam ameondoka na ushindi wa jumla wa penati 9 dhidi ya 8 za Yanga.

Kwa matokeo hayo Yanga imeuvua rasmi ubingwa wake ilioutwaa mwaka jana visiwani humo,huku Azam mabingwa mara nyingi wa michuano hiyo akimsubiri mshindi kati ya Simba sc dhidi ya Namungo fc saa mbili na robo usiku kukutana nae katika fainali itakayofanyika Januari 13 siku ya Jumatano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka