Connect with us

Soka

Yanga Yatua Usiku

Timu ya soka ya Yanga sc imewasili usiku wa leo kutoka nchini Botswana ilipokua imeenda kukipiga na Township Rollers mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0.

Timu hiyo ambao ni mabingwa mara 27 wa ligi kuu Tanzania bara wametua nchini saa saba usiku na kulakiwa na mashabiki wa timu hiyo ambao walijitokeza kuwapokea baada  ya kuwa wamefanikiwa kufuzu kwende raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo watakutana na Zesco united ya Zambia.

Baada ya kutua timu hiyo iliunganisha kambini katika hotel ya Nefaland iliyopo Manzese jijini Dar es salaam ili kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu shooting utakaopigwa siku ya jumatano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka